Baada ya Ronaldo kupiga hat-trick dhidi ya Wolfsburg na kuisaidia klabu yake ya Real Madrid kuvuka hatua ya robo fainali na kutinga nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, mtaani imekuwa ni gumzo kila kona kila ofizi vijiweni na sehemu mblambali hadi maofisini.
Kwa mujibu wa matandao wa sokkaa, hii ndiyo top ten ya hat-trick za kukukumbukwa zaidi kwenye michuano ya Champions League.
10. Mario Gomez vs FC Basel, March 2012
Mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich licha ya kuihama klabu hiyo, lakini jina lake litaendelea kukumbukwa kwenye historia ya vitabu vya klabu hiyo.
The Bavarians ilianza kampeni zake kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya mwaka 2012 kwa kupoteza mchezo kwanza wakiwa ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Basel.
Mchezo wa marudiano iliandikwa historia mpya, Robben na Ribbery walikuwa hawakamatiki kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Alianz Arena. Nyota wa mchezo huo alikuwa ni Gomez ambaye alikamilisha hat-trick ndani ya dakika 23. Lakini mwisho wa siku miamba hiyo ya Bundesliga iliangukia pua kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Chelsea.
9. Thiery Henry vs Roma, November 2002
Msimu wa 2002/2003 klabu bingwa Ulaya, Mfaransa huyo aliibeba Arsenal kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya klabu ya AS Roma ya Italia akifanikiwa kupachika bao tatu wavuni timu yake ikitoka na ushindi wa magoli 3-1. Kiwango chake kwenye usiku huo kilikuwa mwiba kwa timu ya Romba mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.
8. Kaka vs Anderlecht, November 2006
Kiungo mchezeshaji wa kibrazil Kaka atakuwa anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa akiwa amevalia uzi wa AC Milan.
Many will remember his demolition of Manchester United at Old Trafford few years ago. One of the greatest moment was against Anderlecht. He bagged his hat-trick in a 4-1 win to give AC Milan hope of progressing to the knock out stage.
Wengi watamkumbuka kwa tukio la kuiangamiza Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford miaka kadhaa iliyopita. Moja ya matukio ya kukumbukwa ni hat-trick yake dhidi ya Anderlecht wakati AC Milan ikishinda kwa bao 4-1na kufufua matumaini ya kusonga mbele kwenye hatua ya mtoano.
7. Wayne Rooney vs Fenerbache, September 2004
Nahodha huyu wa Manchester United alicheza mchezo wake wa kwanza wa klabu bingwa Ulaya September 28, 2004 dhidi ya Fenerbache na kufunga hat-trick yake ya kwanza kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya ngazi ya vilabu.
Wakati huo Rooney alikuwa na miaka 18 na kumfanya kuwa miongoni mwa wenye umri mdogo zaidi kufunga hat-trick kwenye michuano hiyo.
6. Ronaldinho vs Udinese, September 2005
Kwenye wakati wake Ronaldinho hakuwa tu mburudishaji kwenye upande wa soka bali alikuwa mchezaji mwenye uwezo wa kufanya chochote uwanjani. Wakati wowote alikuwa anaweza akamuacha beki kwa chenga za maudhi na kutoa pande la goli au yeye mwenyewe kuzama kambani.
Hat-trick yake dhidi ya Udinese ni moja kati ya nyakati za kukumbukwa zaidi kwenye michuano ya Ulaya.
5. Lionel Messi vs Leverkusen, March 2012
Kwa muda mrefu mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi amekuwa akitawala mihuano ya Champions League , muargentina huyu anauwezo mkubwa wa kuichambua safu za ulinzi za timu nyingi.
Messi alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli matano kwenye mechi moja ya Champions League. Barcelona ilishinda kwa magoli 7-1 kwenye usiku huo na ushindi wa jumla (aggregate) ilikua ni magoli 10-1.
4. Cristiano Ronaldo vs Ajax, October 2012
Ukizungumzia maajabu ya Lionel Messin kwenye michuano ya Ulaya huwezi kuacha kutaja uwezo wa mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United alikuwa hazuiliki na akafanikiwa kutumbukia nyavuni mara tatu kwenye mchezo ambao Madrid ilishinda kwa magoli 4-1 dhidi ya mabingwa wa Uholanzi Ajax Amsterdam
3. Ronaldo vs Manchester United, April 2003
Raia huyu wa Brazil anayefahamika zaidi kwa jina la El Phenomeno alipiga hat-trick dhidi ya Manchester United na kuisaidia timu yake kutinga hatua ya nusu fainali ya Chamipons League mwaka 2003.
Jambo la kukumbukwa zaidi ni pale wakati anatoka uwanjani baada ya kufanyiwa sub dakika ya 65, umati wote wa Old Trafford ulisimama kumshangilia pamoja na mashabiki wa United.
2. Lionel Messi vs Arsenal, April 2010
Mwaka 2010 kwenye mchezo wa robo fainali ya pili, Messi pekeyake alitosha kuiangamiza Arsenal kwa kutandika magoli manne na kuivusha timu yake hadi hatua ya nusu fainali.
- Ronaldo vs Wolfsburg, March 2016
Usiku wa April 12 nyota wa Real Madrid alikuwa hazuiliki. alifunga magoli matatu dhidi ya Wolfsburg na kuisaidia timu yake kupindua matokeo ya mchezo wa kwanza ya kipigo cha bao 2-0 wakiwa ugenini.
Comments
Post a Comment