SIR ALEX FERGUSON ALICHEMKA KUMWACHIA PAUL POBGA ...aliiondoka bure lakini leo thamani yake ni pauni mil 100
Paul Pogba anawindwa na Barcelona katika kipindi hiki ambacho inaonekana yupo tayari kuondoka Juventus kiangazi hiki.
Kwa sasa Pobga kinda wa zamani wa Manchester United anatajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 100, hatua inayowafanya wachambuzi wa soka waamini kuwa kocha wa zamani wa United Sir Alex Ferguson alifanya kosa kubwa kumwacha nyota huyo aondoke bure.
Akiwa Manchester United, Pobga hakupewa nafasi na Ferguson ya kuanza katika mchezo wowote ule wa timu ya wakubwa zaidi ya kucheza mechi chache sana akitokea benchi.
Kiungo huyo akaamua kutimka na kujinga na Juventus mwaka 2012 na kuibuka kuwa shujaa aliyeweza kucheza mechi 121 na kufunga magoli 28.
United ni moja ya timu za Ulaya zinazotajwa kuwania saini ya Pobga lakini mashabiki wake wengi wamekuwa wakiumizwa na matamanio ya klabu yao kutaka kumwaga pesa ndefu kwa mchezaji waliyempuuza na kumwacha aondoke bure.
Enzi hizo: Paul Pogba (wa pili kushoto), aliondoka Manchester United bila kuanza katika mechi yoyote ya wakubwa lakini sasa ni mchezaji lulu duniani anayetamaniwa na vilabu vyote vikubwa barani Ulaya. Picha hii ni ya mwaka 2011 baada ya kushinda kombe la FA la Vijana FA. Wengine pichani Ryan Tunnicliffe (kushoto), Jesse Lingard wa pili kushoto na Ravel Morrison
Inadaiwa Ferguson alikataa wazo la wakala wa Pobga aliyetaka mchezaji wake alipwe pauni 20,000. Pichani ni Pogba akicheza mechi ya Premier League dhidi ya West Brom 2012
Comments
Post a Comment