SHAW AMPA ‘SHAVU’ DE GEA KUPITIA TWITTER


SHAW AMPA 'SHAVU' DE GEA KUPITIA TWITTER

Shaw-De Gea

Luke Shaw kwa sasa amekuwa mtazamaji wa mechi za Man United bada ya kuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kukipiga, full-back huyo alivunjika vibaya mguu wake kwenye mchezo wa Champions League kati ya Manchester United dhidi ya PSV September mwaka jana na amekuwa akiendelea vizuri wakati huu.

Kunauwezekano Shaw akarejea uwanjani kabla ya msimu huu kumalizika na anaweza akacheza kwenye mchezo wa fainali ya FA Cup endapo timu yake itafanikiwa kufuzu.

Alikuwa makini akiufatilia mchezo wa United dhidi ya West Ham na hakuwashangaza mashabiki alipomtaja mchezaji wake bora wa mchezo 'Man of the Match' kwa tweet yake iliyosomeka 'David De Gea'.

Shaw

Shaw-De Gea 1

Shaw alimpa heshima hiyo mlinzi mwenzake (golikipa) De Gea badala ya wafungaji wa magoli kwenye mchezo huo (Rashford and Fellaini).

Baada ya kuwa nje karibu msimu mzima, Shaw amejifunza mengi namna ya kuusoma mchezo na kuwapongeza wale wote wanaofanya vizuri.

Manchester United itakutana na Everton kwenye mchezo wa nusu fainali ya FA Cup kwenye uwanja wa Wembley baada ya kuichapa West Ham kwa bao 2-1 kwenye mchezo wa marudiano hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kufuatia timu hizo kutoka sare kwenye mchezo wa kwanza.

Mambo muhimu ya kufahamu:

  • Manchester United imefika hatua ya nusu fainali ya FA Cup kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011.
  • Tangu Marcus Rashford aanze kucheza kwenye kikosi cha Manchester United, amefunga magoli sita kwenye mechi 11. Hakuna mchezi mwingine wa United mwenye zaidi ya magoli matatu.
  • Marouane Fellaini amefungia Manchester United goli la kwanza tangu alipofanya hivyo December zikiwa zimepita mechi 12 bila kutupia kambani.
  • West Ham sasa wamefikisha mechi 12 bila uhindi kwenye mashindano yote dhidi ya (D5 L7).


Comments