ROONEY MWANAMICHEZO TAJIRI ZAIDI UINGEREZA ...GARETH BALE, FALCAO, AGUREO, HAZARD NA FABREGAS NAO WAMO
Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Times la England Wayne Rooney, ndiye mwanasoka kijana tajiri zaidi Uingereza kwa mwaka 2016.
Rooney mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni nahodha wa Manchester United na timu ya taifa ya England ameingiza faida ya pauni milioni 82, ikiwa ni ongezeko la pauni milioni 10 kutoka mwaka uliopita na hivyo kuwa mwanamichezo aliyeingiza mkwanja mrefu zaidi kwa wanamichezo wenye umri chini ya miaka 30.
Nyota huyo ameingiza pesa hizo kutokana na mshahara wake wa pauni 300,000 kwa wiki anaolipwa Manchester United sambamba na mikataba ya biashara kupitia Nike na Sumsung.
Rooney anaongoza orodha hiyo inayojumuisha wanamichezo wa Uingereza popote pale duniani pamoja na wale kigeni lakini waonafanya kazi zao ndani ya Uingereza.
Nyota wa tenis Andy Murray anashika nafasi ya pili kwa kuingiza pauni 58 akiwa amefungana na mkali mwingine wa tenis Jamie Murray.
Katika orodha hiyo, wako wanasoka Gareth Bale, Samir Nasir, Falcao, Eden Hazard, Cesc Fabregas na Sergio Aguero.
Wayne Rooney ndiye mwanamichezo tajiri zaidi Uingereza
Nyota wa tenis Andy Murray anashika namba mbili
Mkali wa golf Rory McIlroy saw his wealth increase by £18m over the past year to make a total of £56m
KWA MUJIBU WA SUNDAY TIMES HAWA NDIO WANAMICHEZO VIJANA MATAJIRI ZAIDI UINGEREZA KWA MWAKA 2016
1 Wayne Rooney Football, Manchester United £82
2 Andy and Jamie Murray Tennis £58m
3 Rory McIlroy Golf £56m
4 Gareth Bale Football, Real Madrid £34m
5 Sergio Aguero Football, Manchester City £33m
6 David Silva Football, Manchester City £31m
7= Cesc Fabregas Football, Chelsea £29m
7= Radamel Falcao Football, Chelsea £29m
9 Samir Nasri Football, Manchester City £22m
10= Eden Hazard Football, Chelsea £18m
10= Amir Khan Boxing £18m
Comments
Post a Comment