Cristiano Ronaldo anatarajiwa kukosa mchezo La Liga kwa mara ya kwanza msimu huu Jumamosi hii dhidi ya Rayo Vallecano, hiyo ni baada ya kupata maumivu ya msuli katikati ya wiki.
Kinara huyo wa magoli katika historia ya Real Madrid amecheza michezo yote 34 ya La Liga na mechi 10 za Champions League kabla ya kuumia kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Villarreal Jumatano usiku.
Ronaldo anakaa benchi kwenye mchezo wa Rayo ili kuhakikisha anakuwa fiti kwa mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa itakayowakutanisha na Manchester City Jumanne usiku.
Comments
Post a Comment