Mwanasoka nyota wa Leicester City Riyad Mahrez ametwaa tuzo ya mwanasoka bora (PFA Player) wa mwaka 2016.
Mahrez amekuwa na msimu mzuri akiisaidia timu yake kung'ang'ania kileleni mwa Premier League baada ya kuifungia magoli 17 na kupika magoli 11.
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Algeira ametwaa tuzo hiyo ambayo msimu uliopita ilikwenda kwa Eden Hazard wa Chelsea.
Mahrez ametoa shukrani kwa wachezaji wenzake wa Leicester City huku akisema bila wao yeye si lolote.
Nyota wa Leicester City Riyad Mahrez akipozi na tuzo yake
Mahrez katika picha ya pamoja na kocha wa Leicester City Claudio Ranieri (kushoto)
Mahrez akishuruku wachezaji wenzake
Comments
Post a Comment