REAL MADRID inatafuta            kuandika rekodi ya kihistoria katika La Liga, ya kushinda            mfululizo mechi 12 za mwisho, mafanikio ambayo hayajafikiwa na            timu nyingine yoyote.
        Tayari Madrid imeshinda            mechi nane mfululizo dhidi ya Levante, Celta, Las Palmas,            Sevilla, Barcelona, Eibar, Getafe na Villarreal, ikibakiwa na            mechi nne dhidi ya Rayo Vallecano, Real Sociedad, Valencia na            Deportivo La Coruna.
        Timu ya kwanza kuandika            rekodi ya kushinda mechi nyingi mfululizo mwishoni mwa msimu            wa ligi ni Barcelona iliyofanya hivyo msimu wa 1959/60 ambapo            ilishinda mechi zake nane za mwisho.
        Barcelona ambayo kabla            ya kushinda mechi hizo ilikuwa nafasi ya pili katika msimamo            wa ligi, ilimaliza ikiwa bingwa.
        Villarreal iliifikia            rekodi hiyo ya Barcelona msimu wa 2006/07, ambapo ikiwa            katikati ya msimamo ilishinda mfululizo mechi nane za mwisho            na kupanda hadi katika nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya.
        Real Madrid ikiwa katika            ubora wake, ilifanikiwa kushinda mfululizo mechi saba za            mwisho na kumaliza ikiwa bingwa wa ligi mara mbili katika            misimu ya 1980/81 na 2011/12.
        
Comments
Post a Comment