REAL MADRID WAANZISHA VITA VYA MANENO NA ATLETICO MADRID CHAMPIONS LEAGUE



REAL MADRID WAANZISHA VITA VYA MANENO NA ATLETICO MADRID CHAMPIONS LEAGUE

RAIS wa zamani wa Real Madrid, Lorenzo Sanz, amekoleza 'vita' kati ya timu yake na Atletico Madrid msimu huu, kwa kueleza kuwa anawataka wapinzani wao hao wa mji mmoja katika fainali ya Champions League kwa kuwa ni rahisi kuwafunga.

Klabu hizo mbili kwa sasa zinapigana vita inayofanana, kila moja ikijaribu kutwaa taji la La Liga kutoka kwa Barcelona na pia kufika fainali ya Champions League.

Sanz, ambaye alikuwa rais wa Real kutoka 1985 hadi 1995 na kuwa mwenyekiti kutoka 1995 hadi 2000, alifanikiwa kupata mafanikio wakati timu hiyo iliposhinda Champions League mwaka 1998 na 2000.

Na sasa Mhispania huyo anaamini kwamba fainali inayowezekana kati ya Real na Atletico itamalizika kwa matokeo ya aina moja tu – ushindi kwa Real.

"Natarajia Atletico itafika fainali ya Champions League kwa sababu tunaweza kuwafunga… Tutashinda taji la 11 (Champions League)," alisema Sanz akijiamini.


Comments