WAYNE Rooney amemkuna Louis van Gaal aliposhika dimba la kati katika mechi ambayo Manchester United wameshinda 2-0 dhidi ya Crystal Palace Jumatano usiku, na sasa nafasi hiyo inamuhusu straika huyo.
Kutokana na kumthibitisha Marcus Rashford kuwa chaguo la kwanza katika nafasi ya mshambuliaji wa kati, Van Gaal amekiri kuwa amelazimika kumtafutia Rooney majukumu mengine katika nusu fainali ya FA Cup dhidi ya timu yake ya zamani ya Everton Jumamosi.
"Hakuna mchezaji mwenye nafasi ya kudumu, natumia wachezaji ambapo nadhani wanaweza kutoa mchango mkubwa zaidi katika mechi fulani. (Rooney) alikuwa na jukumu kwenye kiungo kutokana na namna Crystal Palace walivyocheza.
"Sitaki kumbadili (Marcus) Rashford kama straika. Inabidi kuangalia nafasi nyingine kwa Wayne. Alifanya hivyo mwaka uliopita (kucheza kiungo), hivyo si jambo jipya kwangu. Nina furaha sana kwa jinsi alivyocheza," alisema Van Gaal.
Comments
Post a Comment