Ikiwa imeshajihakikishia kumaliza katika nafasi tatu za juu, kocha wa Leicester City Claudio Ranieri anaamini klabu yake itatwaa ubingwa wa England.
Vinara hao wa ligi wamekuwa na kampeni nzuri ya kushinda taji hilo na sasa wako pointi tano juu ya Tottenham huku zikiwa zimesalia mechi nne kabla ya ligi kufika ukingoni.
Leicester wanaikaribisha Swansea Jumapili hii katika mechi ambayo iwapo watashinda, watakuwa wamezidi kuligusa taji la Premier League.
Ranieri anasema kuwa lengo lake kuu sasa ni kushinda taji la ligi.''Ni mwaka huu ama isifanyike tena'' alisema kocha huyo akimaanisha kuwa nafasi waliyonayo inaweza kutokea mara moja katika maisha yote.
''Tumefanikiwa kufuzu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao, ni ufanisi mkubwa kwa kila mtu lakini sasa tunajaribu kushinda taji la ligi na nguvu zetu zote.
"Nimewaambia wachezaji wangu kwamba sasa ndio wakati mzuri wa kuweka nguvu zote. Tunahitaji pointi nane tushinde taji na na tutajaribu kufanya hivyo.
Comments
Post a Comment