Msiba wa mwanamuziki Ndanda Kosovo aliyefariki Jumamosi asubuhi, umeendelea kuteka hisia za watu wengi.
Ndanda anazikiwa Jumatano hii saa 9 mchana kwenye makaburi ya Kinondoni (Mwembejini) walikozikwa mastaa wengine kama Steven Kanumba, Adam Kuambiana, Martin Kasyanju na wengine wengi.
Watu wamekuwa wakiwasili kila wakati kwenye eneo la msiba Kinondoni Hananasif kwenye nyumba ya balozi wa Congo (DRC).
Ratiba kamili ya kamili ya mazishi ya Ndanda ni kama hivi:
Jumatano (13-APR-2016) saa 1 Asubuhi: Kwenda kuchukua mwili Muhimbili Hospital
Saa 4 asubuhi: Mwili kuwasili Kinondoni msibani.
Saa 6 Mchana: Chakula
Saa 7 mchana: Kuaga Mwili
Saa 9 mchana: Makaburini (Kinondoni)
Wageni wa heshima wanaotarajiwa kuhudhuria mazishi ni: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye, balozi wa Congo nchini Jean Pierre Mutamba na maafisa wote wote wa ubalozi wa Congo DRC.
PATA PICHA 18 ZA WATU WALIOKUWEPO MSIBANI JUMANNE USIKU
Asha Baraka na Juma Mbizo
Meneja wa Twanga Pepeta Hassan Rehani (kushoto) akiwa na Khamis Dacota wa Clouds FM
Kutoka kushoto ni Pablo Masai, Doyi Moke na Joniko Flower
Marapa G7 wa FM Academia na kulia ni Mirinda Nyeusi wa Mashujaa Band
Kutoka kushoto ni Mirinda Nyeusi, Hassan Rehani na Haji BSS
Jose Mara na Asha Baraka
Baadhi ya waombolezaji wa kike waliofika msibani Jumanne usiku
Wanenguaji wa FM Academia
Mwimbaji wa FM Academia Malu Stonch ambaye aliingia Tanzania pamoja na marehemu Ndanda
Kutoka kushoto ni Totoo ze Bingwa, Jose Mara, Juma Mbizo na Richard Mangustino
Mahema yalivyokuwa yakitayarishwa
Mule Mule FBI
Kushoto ni Pishuu Meshaa akiwa na Steve
Kushoto ni rapa Sauti ya Radi
Comedian Steve Nyerere
Mtangazaji wa Chanel Ten Sunday Mwakanosya
Wadau
Baadhi ya waombolezaji
Comments
Post a Comment