PEP GUARDIOLA KUMPELEKA MIKEL ARTETA MANCHESTER CITY


PEP GUARDIOLA KUMPELEKA MIKEL ARTETA MANCHESTER CITY
Mikel Arteta could be            offered a first-team coaching role by incoming Manchester City            boss Pep Guardiola
KIUNGO wa Arsenal, Mikel Arteta anaweza kujiunga na Manchester City kama sehemu ya benchi la ufundi la Pep Guardiola.

Arteta mwenye umri wa miaka 34, atakuwa nje ya mkataba mwisho wa msimu na amekusudia kustaafu na kuhamia katika ukocha kiangazi hiki kutokana na matatizo ya kuumia hivi karibuni.

Licha ya kuwa nahodha, ushiriki wa kiungo huyo Mhispania katika kikosi cha Arsene Wenger umezingirwa na vikwazo katika kipindi cha misimu miwili ya mwisho kutokana na idadi ya kuwa majeruhi, akicheza mechi nane za Premier League msimu huu kwa sababu ya  kuendelea kwa tatizo hilo.

Arteta tayari amejipanga kuhamia katika kufundisha soka na amekamilisha baadhi ya kozi za ukocha katika chuo cha soka cha Arsenal.

Guardiola anajiandaa kwenda na timu yake ya ufundi Etihad Stadium kiangazi hiki wakati atakapochukua nafasi ya Manuel Pellegrini, na chanzo cha habari kimeupasha mtandao wa ESPN FC kwamba yu tayari kumpa ofa Arteta kuwa miongoni mwa wasaidizi wake.


Wawili hao waliopikwa pamoja katika kituo maarufu cha soka cha Barcelona - La Masia wakiwa wachezaji makinda, ni marafiki wa karibu.


Comments