PEP GUARDIOLA ameamua kufunga mdomo wake akikataa kuzungumzia taarifa za dili la pauni milioni 30 ambalo tayari limedaiwa 'kuiva' kwa ajili ya kumpeleka Manchester City kiungo Ilkay Gundogan wa Borussia Dortmund kiangazi hiki.
Mhispania huyo ambaye atachukua nafasi ya Manuel Pellegrini kama kocha wa City mwisho wa msimu, inaeleweka kuwa aliweka mipango yake ya usajili baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Michezo wa timu hiyo, Txiki Begiristain jijini Amsterdam, Uholanzi mwezi uliopita.
Lakini kocha huyo wa Bayern Munich 'aliruka kimanga' wakati alipotakiwa kutoa maoni yake juu ya tetesi zinazozunguka mustakabali wa Gundogan.
"Mimi ni kocha wa Bayern Munich," alijibu alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu dili la usajili kwa mchezaji huyo wa miaka 25.
Comments
Post a Comment