Pamoja na Kiwango Kibovu Uwanjani – Man Utd yazifunika Barca, Madrid, katika listi ya vilabu vyenye faida kubwa




Pamoja na Kiwango Kibovu Uwanjani – Man Utd yazifunika Barca, Madrid, katika listi ya vilabu vyenye faida kubwa

Mauzo makubwa ya haki ya matangazo ya TV, mauzo ya jezi, mauzo ya wachezaji na uuzaji, matangazo ya biashara na uuzaji wa bidhaa mbalimbali zenye nembo za vilabu ni moja ya mambo yaliyozitengenezea faida kubwa vilabu vya soka kwa muda wa miezi zaidi ya 12 iliyopita.  
 Jarida la Forbes linalodili na masuala ya biashara na fedha limechapisha listi ya vilabu 10 vilivyoingiza faida kubwa duniani kote.

   Pamoja na matokeo yasiyoridhisha uwanjani, klabu ya Manchester United imetajwa na jarida la Forbes la Marekani kuwa klabu iliyoingiza faida kubwa zaidi kwa miezi 12 iliyopita. 

Listi kamili ya vilabu 10 vya soka vyenye faida kubwa.

1. Manchester United: $190 million

2. Real Madrid: $162 million
3. Manchester City: $131 million
4. Arsenal: $122 million
5. Liverpool: $115 million
6. Barcelona: $108 million
7. Juventus: $81 million
8. Tottenham Hotspur: $73 million

9. Schalke: $67 million
10. Bayern Munich: $60 million

 



Comments