Joto la Mourinho kutua Manchester United            bado lipo na sasa inadaiwa kocha huyo mtata, amepanga kutua            Old Trafford na kusajili angalau wachezaji wapya watano katika            kikosi.
        Kwa mujibu wa mtandao wa ESPN, straika            Harry Kane wa Tottenham Hotspur na beki wa kati wa Everton            anayemudu pia beki ya kulia, John Stones wako juu ya orodha ya            Mourinho, lakini pia ameelezea kuthibitisha kutaka kumsainisha            Zlatan Ibrahimovic.
        Kiungo wa Benfica, Renato Sanches pia            anatarajiwa kujiunga na United kiangazi hiki, licha ya            kutakiwa na Arsenal.
        
Comments
Post a Comment