Inter Milan wamefufua matumaini ya kupata nafasi ya kwenda kucheza soka la ulaya msimu ujao baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Udinese juzi jumamosi.
  Katika mchezo huo Inter walifunga magoli yao          kupitia Jovetic aliyefunga mawili na Mauri Icard akifunga          lingine na kuifanya Inter kufikisha  pointi 64 wakishika nafasi          ya 4 nyuma ya Roma wenye pointi 68, huku zikiwa zimebaki mechi 3          ligi kumalizika. 
  Mchezo huu wa Inter vs Udinese pia umeweka          historia mpya katika Serie A, ligi ambayo ina sifa ya kukumbatia          wachezaji wa kiitaliano. Mechi amya leo haijahusisha mchezaji          hata mmoja raia wa Italia katika vikosi vyote viwili vilivyoanza          kwa timu zote mbili. 
Hii haijawahi kutokea katika ligi ya Serie A tangu kuanzishwa          kwake. 
          Takwimu:  Inter Milan – Udinese 
Msimamo wa Ligi
Comments
Post a Comment