Marcus Rashford alikataa kujiunga na Liverpool na kuamua kujiunga na Manchester United wakati alipokuwa na umri wa miaka saba.
Rashford mwenye umri wa miaka 18 ameendelea kuonyesha ubora wake katika msimu wake huu wa kwanza kwa kufunga bao tamu lililochangia ushindi wa bao 2-1 dhidi ya West Ham kwenye mchezo wa FA Jumatano usiku kwenye dimba la Upton Park.
Katika mchezo huo shuti lake likajinyonganyonga na kwenda kujaa wavuni kwenye kona ya juu na kuwa bao lake la sita ndani ya michezo 11 aliyocheza tangu alipocheza mchezo wake wa kwanza kwenye kikosi cha wakubwa cha United mwezi Februari.
Rashford ameweka wazi kuwa United ipo kwenye damu yake tangu utotoni na ndiyo maana aliichagua klabu hiyo na kuipotezea Liverpool
Marcus Rashford kwa mara nyingine tena amefunga bao la kusisimua wakati Manchester United ikiifungaWest Ham 2-1 Jumatano usiku na kutinga nusu fainali ya FA
Kinda huyo wa miaka 18 akifunga bao lake dhidi ya West Ham
Comments
Post a Comment