MARCUS RASHFORD AISHUSHA DARAJA ASTON VILLA ...atupia bao pekee, watamwelewa tu, Rooney arejea rasmi
Marcus Rashford kwa mara nyingine tena anaibeba Manchester United baada ya kuifungia bao pekee kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Aston Villa kwenye uwanja wa Old Trafford.
Kwa bao hilo la dakika ya 32, Aston Villa wanashuka rasmi daraja ikiwa ni mara yao ya kwanza ndani ya miaka 28 iliyopita.
Aston Villa ina pointi 16 ambazo hata kama ikishinda michezo yake iliyosalia, haitawasaidia lolote.
Marcus Rashford mwenye umri wa miaka 18, alifunga bao hilo akiunganisha krosi ya Antonio Valencia.
Nahodha Wayne Rooney alianza katika mchezo huo, akifanya hivyo kwa mara ya kwanza tangu alipoumia katikati ya mwezi Februari.
MANCHESTER UNITED (4-2-3-1): De Gea 6; Valencia 7.5, Smalling 6.5, Blind 6, Rojo 6; Schneiderlin 6, Fellaini 6.5; Mata 6 (Fosu-Mensah 89), Rooney 6.5 (Lingard 67 6), Depay 7; Rashford 7 (Martial 76 6)
ASTON VILLA (4-4-1-1): Guzan 6; Hutton 5.5, Clark 6, Lescott 5.5, Cissokho 5.5; Sinclair 5.5, Bacuna 6, Westwood 6, Richardson 6 (Gestede 82 6.5); Gueye 6; Ayew 6.5
Marcus Rashord anashangilia bao lake
Kitu kinatinga wavuni
Dogo anapongezwa na nahodha wake
Wachezaji wa Aston Villa hoi baada ya kushuka daraja
Comments
Post a Comment