MARCUS RASHFORD AGEUKA KUWA MWOKOZI WA VAN GAAL



MARCUS RASHFORD AGEUKA KUWA MWOKOZI WA VAN GAAL
Manchester United star            Marcus Rashford celebrates after scoring the opener against            West Ham
MARCUS Rashford anaweza kuwa mwokozi wa Louis van Gaal aliyekalia 'kuti kavu' Old Trafford kutokana na kubeba bahati ya Manchester United kushinda kila mechi ambayo anatikisa nyavu za timu pinzani.

Kinda huyo alipiga bao kali Jumatano usiku wakati Manchester United ikishinda mechi ya robo fainali ya FA Cup dhidi ya West Ham.

Rashford amefunga mabao sita katika mechi 11 alizocheza katika mashindano yote, tangu alipopewa jezi kwa mara ya kwanza na Van Gaal dhidi ya Midtjylland ya Denmark, walipokutana mechi ya marudiano ya Europa League Februari mwaka huu ambapo alitupia mara mbili.

Kutokana na kubeba bahati ya United kushinda kila mechi anayofunga, kinda huyo wa miaka 18 amejitengenezea uhakika wa mkataba mpya baada ya huu wa sasa kumalizika mwakani, bila kujali atakuwapo Van Gaal, Jose Mourinho au mwingine yeyote.

Van Gaal anaingia katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba msimu ujao, lakini kuna uwezekano mkubwa akatupiwa virago na nafasi yake kuchukuliwa na Mourinho kutokana na mwenendo mbaya wa timu.


Comments