MANCHESTER UNITED YATENGA MSHAHARA MNONO KWA NEYMAR ILI KUMNG'OA BARCELONA KWA ADA YA REKODI MPYA YA DUNIA



MANCHESTER UNITED YATENGA MSHAHARA MNONO KWA NEYMAR ILI KUMNG'OA BARCELONA KWA ADA YA REKODI MPYA YA DUNIA
Barcelona did not want            Neymar to play in two international tournaments this summer -            and now he will not
MANCHESTER UNITED imeripotiwa "kukaa mkao wa kula" wakati Barcelona ikielezwa kuwa tayari kumwachia straika wake nyota, Neymar aondoke katika klabu hiyo.

Klabu hiyo ya England kwa muda mrefu imekuwa ikimtamani Mbrazil huyo, na kwa mujibu wa ripoti imekuwa ikiwasiliana na wawakilishi wake kuweka wazi kuwa iko tayari kutimiza matakwa ya mkataba wake Barca kwa kulipa pauni milioni 144.

United pia iko tayari kumpa Neymar mwenye miaka 24 ofa ya mshahara mnono wa pauni 300,000 kwa wiki kama atakubali kuondoka Nou Camp na kutua Old Trafford.

Straika huyo wa zamani wa Santos ya Brazil kwa sasa anavuta mshahara wa pauni 77,000 kwa wiki Barca, hivyo atapandishiwa karibu mara tatu zaidi kama ataamua kuhamia United.

Hata hivyo, The Sun limeripoti kuwa uamuzi wa Neymar utategemea majaliwa ya United kama itafuzu Champions League msimu ujao, kitu ambacho bado hakina uhakika kwa sasa ambapo imeachwa nyuma pointi mbili na wapinzani wao wa mji mmoja Manchester City katika mbio za kuwania 'top four'.

Bado kuna matumaini kwa United kufanikiwa dili hili wakati Barcelona ikihofia kutoweza kukidhi mahitaji ya Neymar kifedha bila kuiweka klabu katika hatari, wakati pia ikikabiliwa na kibarua cha kuwabakisha mastaa wengine kama Lionel Messi na Luis Suarez kwa kuwapa mikataba mipya.


Comments