MANCHESTER UNITED YAICHAPA EVERTON 2-1 NA KUTINGA FAINALI YA FA CUP ...Martial aibuka shujaa, Lukaku akosa penalti
Manchester United imetinga fainali ya FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007 baada ya kuifunga Everton 2-1 kwenye nusu fainali iliyopigwa katika dimba la Wembley.
Marouane Fellaini aliifungia United bao la kwanza dhidi ya timu yake hiyo ya zamani kunako dakika ya 34.
Kipindi cha pili Everton ilipoteza nafasi nzuri ya kusawazisha pale Romelu Lukaku alipopiga penalti iliyopanguliwa na kipa David De Gea.
Hata hivyo dakika ya 76 Chris Smalling alijifunga na kufanya matokeo yawe 1-1 hadi dakika za majeruhi ambapo Anthony Martial alikimbia na kuuwahi mpira wa Ander Herrera na kufunga bao la ushindi kwa United.
United sasa itaumana na mshindi wa Jumapili kati ya Crystal Palace na Watford.
Everton: Robles, Besic, Stones, Jagielka, Baines, McCarthy, Gibson (Mirallas 90mins), Lennon (Deulofeu 70), Barkley, Cleverley, Lukaku
Manchester United: De Gea, Fosu-Mensah (Valencia 62), Smalling, Blind, Rojo, Carrick, Lingard, Fellaini (Herrera 87), Rooney, Martial, Rashford
Anthony Martial akishangilia bao la ushindi alilifunga dakika za majeruhi
Martial akiifungia United bao la ushindi
Nahodha Wayne Rooney akishangilia baada ya mpira kwisha
Louis van Gaal na Anthony Martial wakifurahi baada ya mpira kumalizika
Nyota wa Everton Gerard Deulofeu na Tom Cleverley wakishangilia baada ya Smalling kujifunga na kuwa bao la kusawazisha
Marouane Fellaini akisherehekea bao lake dhidi ya timu yake ya zamani
Comments
Post a Comment