MANCHESTER UNITED YAFUFUA MBIO ZA TOP 4


MANCHESTER UNITED YAFUFUA MBIO ZA TOP 4

Man United vs Palace

Goli la kwanza la United lilipatikana kutokana na Damien Delaney kujifunga wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa krosi iliyochongwa na Matteo Darmian.

Manchester United imesogea na kukaa nyuma ya Arsenal kwa pointi moja, ikiwa imesaliwa na mechi nne za Premier League msimu huu, Man United imepata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Crystal Palace na kujiimarisha katika nafasi ya tano nyumama ya The Gunners iliyo nafasi ya nne ikiwa imesaliwa na michezo mitano ya ligi.

Golikipa wa Palace Julian Speroni aliendelea kuiweka timu yake mchezo kwa kuokoa michomo kadhaa kabla ya Darmian hajapachika bao la pili  kwa mkwaju mkali akiwa umbali wa mita 20 toka golini.

Arsenal wenye game moja mkononi watamenyana na West Brom siku ya Alhamisi katika mwendlezo wa ligi ya EPL.

Damian amefunga goli lake la kwanza tangu amejiunga na United na kukipa ushindi kikokosi cha Louis van Gaal kwenye usiku ambao mashabiki wengi wa timu hiyo hawakujitokeza uwanjani kushuhudia mechi huku viti vingi vikionekana vikiwa havina watu.

United itaweza kufuzu michuano ya Champions League?

Mchezo huo ulikuwa ni muhimu kwa United kushinda na wakaweza kufanya hivyo dhidi ya Palace dhaifu ambayo inapambana kujikwamua kutoka kwenye nafasi za chini za kukwepa kushuka daraja.

Ushindi wa mechi hiyo bado haumaanishi kwamba United imekuwa na kwenye wakati mbaya katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu, huku kikosi hicho cha Van Gaal kikiwa kimejipa kazi ya kupambana kuhakikisha kinamaliza ligi kikiwa kwenye nafasi nne za juu ili kufuzu kucheza michuano ya Champions League msimu ujao.

United inaratiba ngumu ikiwa inatarajia kukutana dhidi ya vinara wa ligi hiyo Leicester City (uwanja wa nyumbani) na West Ham (ugenini) baadaye watatakiwa kusafiri kuifuata Norwich ambayo inapambana kusalia kwenye Premier League kabla haijamalizana dhidi ya Bournemouth kwenye mchezo wa mwisho utakaopigwa Old Trafford.



Comments