MANCHESTER UNITED KUIPIKU JUVENTUS KWA KIUNGO BERNARDO SILVA WA MONACO


MANCHESTER UNITED KUIPIKU JUVENTUS KWA KIUNGO BERNARDO SILVA WA MONACO

MANCHESTER UNITED inapanga kuipiku Juventus katika usajili wa kiungo Mreno, Bernardo Silva wa Monaco katika dirisha la usajili wa kiangazi hiki.

Bernardo amepiga mabao 15 katika mechi 81 akiwa na Monaco tangu alipoichezea kwa mara ya kwanza timu hiyo ya Ligue 1 mwaka 2015.

Gazeti la Tuttosport la Italia linaripoti kuwa Red Devils imeingia katika mbio za kumsajili Bernardo baada ya Juve kumkosa staa huyo wa miaka 21, Januari mwaka huu.

Inafahamika kuwa Monaco walitaka karibu pauni milioni 16 kwa staa huyo wa kimataifa wa Ureno, lakini Old Lady hawakuwa wamejiandaa kulipa fedha hizo.

Ripoti zinasema sasa United imeamua kumfukuzia Bernardo, sambamba na viungo wenzake wawili, Renato Sanches na Andre Gomes.


Comments