MANCHESTER CITY YAHITAJI SARE YA MAGOLI KUITOA REAL MADRID …Etihad yashuhudia sare ya 0-0



MANCHESTER CITY YAHITAJI SARE YA MAGOLI KUITOA REAL MADRID …Etihad yashuhudia sare ya 0-0

Manchester City imeanza kwa sare ya 0-0 kwenye uwanja wake wa Etihad dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Champions League.

Hiyo inamaanisha kuwa katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, miamba hiyo ya England itahitaji sare yoyote ya magoli ili kutinga fainali kwa faida ya goli la ugenini.

Real Madrid wana mlima mrefu wa kupanda nyumbani kwani ni lazima washinde mchezo huo, vinginevyo sare ya 0-0 italazimisha mshindi kupatikana kwa hatua ya matuta.

Hata hivyo Real Madrid wanaweza wakawa na faida ya uwepo wa Cristiano Ronaldo ambaye ameukosa mchezo wa kwanza baada ya kocha wake Zinedine Zidane kuamua kuendelea kumlinda kufuatia maumivu ya msuli aliyoyapata tangu wiki iliyopita.

Awali Zidane alisema Ronaldo yuko fiti lakini mwisho wa siku kocha huyo hakutaka kucheza kamari juu ya afya ya mchezaji huyo tegemeo.




Comments