Manchester City            imefanya mauaji kwenye Premier League baada ya kuicharaza            Stoke City 4-0 ndani ya Etihad Stadium.
        Ushindi huo            unachagiza ari ya timu hiyo kuelekea kwenye nusu fainali ya            Ligi ya Mabingwa Jumanne ijayo dhidi ya Real Madrid.
        Lakini pia ushindi            huo unafanya vita vya timu zinazosaka nafasi ya Top Four            kwenye Premier League kuwa kali.
        Magoli ya            Manchester City yalifungwa na Fernando, Sergio              Aguero aliyefunga kwa mkwaju wa penalti na Iheanacho kinda              wa Kinigeria aliyetikisa nyavu mara mbili.
        Manchester City (4-4-2): Hart            7; Zabaleta 6.5, Mangala 6.5, Otamendi 7, Kolarov 6; Navas 7,            Toure 6.5, Fernando 7 (Demichelis 72, 6), Silva 6.5 (Delph 57,            6.5); Iheanacho 8, Aguero 7 (Bony 65, 6.5) 
        Stoke (4-2-3-1): Given            5.5 (Haugaard 46, 5); Bardsley 6, Shawcross 5, Wollscheid 5,            Muniesa 5.5; Whelan 6, Cameron 5.5; Diouf 6, Imbula 6.5,            Arnautovic 7 (Adam 76, 6); Joselu 4.5
        
Comments
Post a Comment