Manchester City imetinga hatua ya nusu fainali ya Champions League kwa mara ya kwanza baada ya Kevin de Bruyne kupachika bao dakika za lala salama na kuipa City ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Paris St-Germain.
Baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Paris juma lililopita, mchezo bado ulikuwa wazi lakini Sergio Aguero akakosa penati na kuinyima City bao la kuongoza kipindi cha kwanza.
Ashukuriwe Joe Hart aliyeikoa City kwa kufanya saves tatu za hatari na kuendelea luyafanya matokeo kuwa 0-0, mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Zlatan Ibrahimovic ulikuwa hatari zaidi lakini golikipa huyo wa England aliokoa na kuiweka timu yake salama.
Uwanja wa Etihad ukiwa umejazwa na watazamaji takribani 53,039 walishuhudia City ikiweka historia mpya kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya ya kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kiki ya De Bruyne kujaa wavuni dakika 15 kabla ya mchezo kumalizika.
Filimbi ya mwisho iliibua hisia kali kwa mashabiki wa City ambao walijaa kwenye uwanja wa Etihad baada ya kuwa kuwa kwenye mashaka ya kwamba huenda timu yao ingepoteza mchezo huo kutokana na kosakosa za PSG langoni kwa timu yao.
Wawakilishi hao pekee wa England katika michuano ya Champions League walikuwa hawajawahi kufika hatua ya robo fainali kabla ya msimu huu, sasa wanaweza wakaanza kuiota fainali ya michuano hiyo itakayopigwa jijini Milan msimu huu.
Sasa wanasubiri draw ambayo itafanyika Ijumaa kujua watakutana na timu gani kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi wa jumla wa magoli 3-2 kwenye mchezo uliobatizwa jina la 'vita ya matajiri wa Ulaya'.
Takwimu unazotakiwa kuzifahamu
- Manchester City imekuwa klabu ya 10 kutoka England kutinga hatua ya nusu fainali ya Champions League/European Cup (baada ya Arsenal, Aston Villa, Chelsea, Derby, Leeds, Liverpool, Manchester United, Nottingham Forest and Tottenham).
- City ni klabu ya nne kutoka EPL kutinga hatua ya nusu fainali ya Champions League tangu mwaka 2010-2011 (klabu nyingine ni Manchester United 2010-11, Chelsea 2011-12, Chelsea 2013-14).
- Kevin de Bruyne amehusika kwenye magoli 27 ya Manchester City kwenye mashindano yote msimu huu (amefunga magoli 15 na ku-assist magoli 12)
- PSG imekuwa ikitupwa nje ya michuano ya Champions League kwenye hatua ya robo fainali mara nne ndani ya misimu minne.
- PSG imeshinda mchezo mmoja kati ya michezo nane iliyocheza ugenini dhidi ya timu za England (W1 D3 L4).
Angalia video ya highlights za mchezo wa Manchester City vs PSG
Comments
Post a Comment