LOUIS VAN GAAL amesema kuibuka kwa straika            wake kinda Marcus Rashford, kunarandana na ilivyokuwa kwa            Patrick Kluivert katika klabu ya Ajax Amsterdam ya Uholanzi.
        Mholanzi huyo ambaye alikuwa kocha wa Ajax            wakati Kluivert alipoibuka kwa mara ya kwanza na kutikisa            katika Eredivisie, anadhani Rashford anaweza kufuata nyayo za            straika huyo wa zamani wa Newcastle United.
        Akiwa na mabao saba katika mechi 13 msimu            huu, kinda huyo wa miaka 18 ametikisa katika Premier League            wakati nyota wenzake wanaomzunguka wakihangaika kuwa kwenye            kiwango.
        "Ana umbile sawa na Patrick, lakini            Patrick alikuwa vizuri sana katika uzito wa mwili, lakini            nadhani hiyo ni sula la muda tu kwa Rashford," alisema van            Gaal.
         "Lakini            vipi alikuwa Kluivert katika mwaka wangu wa kwanza Ajax ndivyo            ilivyo kwa Rashford sasa katika mwaka wangu wa pili United."
        Kluivert alikwenda hadi kucheza katika            timu kama Barcelona na AC Milan, sambamba na kufunga mabao 40            katika mechi 79 alizoichezea timu ya taifa ya Uholanzi.
        
Comments
Post a Comment