LIVERPOOL YAMWANIA KINDA WA MAAJABU OUSMANE DEMBELE WA RENNES




LIVERPOOL YAMWANIA KINDA WA MAAJABU OUSMANE DEMBELE WA RENNES

LIVERPOOL imejiunga katika orodha ndefu ya klabu zinazoutolea macho uhamisho wa 'mtoto wa ajabu' wa Rennes ya Ufaransa, Ousmane Dembele.

The Reds ina nia ya kuimarisha safu ya ushambuliaji kiangazi hiki baada ya kuangushwa na Christian Benteke iliyemsajili kwa fedha nyingi mwaka jana, na kwa mujibu wa habari kutoka Ufaransa klabu hiyo imekuwa ikifuatilia mwenendo wake katika wiki za hivi karibuni.

Kinda huyo anaonekana walau anafaa kwenda sambamba na staili ya uchezaji inayopendelewa na Jurgen Klopp, lakini Liverpool ina kibarua cha kupambana kuweza kuzipiku klabu nyingine kubwa kupata saini yake, huku ikiwa haina uwezekano wa kucheza Champions League.

Straika huyo Mfaransa mwenye miaka 18, aliyemudu kupiga mabao 12 katika mechi 21 akiwa na jezi ya Rennes msimu huu, amezitamanisha pia klabu nyingine kubwa barani Ulaya zikiwamo Manchester United, Barcelona na Bayern Munich.


Comments