Liverpool imeisambaratisha vibaya Everton kwa kuibutua bao 4-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa Jumatano usiku katika dimba la Anfield.
Mabao ya Liverpool yalifungwa Divock Origi dakika ya 43, Mamadou Sakhod dakika ya 45, Daniel Sturridge dakika ya 61 na Philippe Coutinho aliyefunga dakika ya 76.
Kwa matokeo hayo, Liverpool yenye pointi 54 huku ikishika nafasi ya saba, inazidi kuwafukuza kimya kimya mahasimu wao Manchester United inayoshikilia nafasi ya tano kwa pointi zake 59. Liverpool ina kiporo cha mchezo mmoja.
Katika mchezo mwingine, West Ham imeifunga Watford 3-1.
Liverpool (4-2-3-1):
Mignolet 6.5, Clyne 7, Lovren 7, Sakho 8, Moreno 7, Lallana 7.5, Milner 8.5 (Ibe 80), Lucas 7, Coutinho 8, Firmino 7 (Allen 66, 6.5), Origi 7.5 (Sturridge 53, 7)
Everton (4-2-3-1):
Robles 6.5, Oviedo 5, Stones 5, (Pienaar 61, 6), Funes Mori 5.5, Baines 5, McCarthy 5, Barry 5 (Besic 45, 6), Lennon 5.5, Barkley 6 (Cleverley 57, 6), Mirallas 6, Lukaku 6
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia bao la Divock Origi
Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool katika hisia zake kali za ushangiliaji
Mamadou Sakho alitupia bao la pili
Comments
Post a Comment