LIVERPOOL YAIBANA BORUSSIA DORTMUND NYUMBANI KWAO ...Divock Origi afunga, Mats Hummels achomoa


LIVERPOOL YAIBANA BORUSSIA DORTMUND NYUMBANI KWAO ...Divock Origi afunga, Mats Hummels achomoa
Kocha Jurgen Klopp ameibana timu yake ya zamani - Borussia Dortmund baada ya Liverpool kulazimisha sare 1-1 katika mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Europa League.

Mshambuliaji Divock Origi aliifungia Liverpool bao la kuongoza dakika ya 36, lakini nahodha wa Dortmund Mats Hummels akaisawazishia timu yake dakika ya 48.

Kwa kufunga bao la ugenini, Liverpool inajiweka sehemu nzuri zaidi katika mchezo wao wa marudiano utakaofanyika Anfield wiki ijayo.

Matokeo ya mechi zingine za Europa League ni:
Athletic Bilbao 1 - 2 Sevilla
Braga 1 - 2 Shakhtar Donetsk
Villarreal 2 - 1 Sparta Prague
Liverpool striker Divock                  Origi (centre) is congratulated by Liverpool team-mate                  Emre Can following his opening goal in the 36th minute
Mshambuliaji wa Liverpool  Divock Origi (katikati) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Liverpool bao la kuongoza dakika ya 36
Jurgen Klopp did not hold                  back on the touchline after seeing Origi score against                  his former side as he punched the air in jubilation
Jurgen Klopp akishangilia bao dhidi ya timu yake ya zamani
Nahodha wa Dortmund  Mats Hummels (kulia) akishangilia baada ya kumtungua kipa Simon Mignolet kwa mpira wa kichwa



Comments