LIVERPOOL NI USHINDI KWENDA MBELE



LIVERPOOL NI USHINDI KWENDA MBELE

Liverpool vs Everton 1

Jurgen Klopp amefanikiwa kupata ushindi mnono kwenye pambano lake la kwanza la Merseyside derby, Mjerumani huyo ameiongoza Liverpool kuichapa Everton kwa magoli 4-0 ukiwa ni ushindi wa tatu mfululizo kwenye Premier League.

Divock Origi na Mamadou walifunga magoli yao kwa vichwa dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.

Everton ilimpoteza Ramiro Funes Mori aliyelimwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Origi ambaye alishindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Daniel Sturridge.

Sturridge akaifungia Liverpool bao la tatu kabla ya Philippe Coutinho kufunga bishara dakika ya 76 na kuipa timu yake ushindi wa kishindo kwenye mchezo wa mahasimu hao.

Mchezo ulivyokuwa

Everton haijafanikiwa kushinda kwenye uwanja wa Anfield tangu mwaka 1999 na wamekuwa wakionekana mara zote timu hiyo imekuwa ikicheza kama haihitaji matokeo chanya pindi inapocheza kwenye dimba hilo.

Majogoo wa jiji walionekana ni timu iliyojipanga kutokana na mashambulizi iliyokuwa ikiyafanya pamoja lakini kazi nzuri ya golikipa wa Everton Joel Roblesiliwafanya wachelewe kupata bao hadi dakika ya 43.

Kutolewa kwa Funes Moris kwa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga Origi kwenye ankle, kulififisha matumaini ya Everton kupambana kugeuza matokeo ya mchezo.

Liverpool imemaliza mchezo ikiwa imepiga mashuti 37 huku mashuti 13 yakiwa ndiyo yamelenga goli wakati Everton walipiga mashuti matatu na hakuna hata moja lililolenga goli.



Comments