LEICESTER CITY YADHIHIRISHA IMEPANIA KUTWAA UBINGWA ENGLAND ...yaichomolea West Ham sekunde za lala salama
Leicester City pungufu, imetoa sare ya 2-2 na West Ham na kuendelea kujitanua kileleni mwa Ligi Kuu ya England.
Jamie Vardy aliifungia Leicester bao la kuongoza dakika ya 18 kabla hajatolewa kwa kadi nyekundu dakika 56 na kupelekea West Ham kupata mabao mawili dakika ya 84 na 86 kupitia kwa Andy Carroll kwa njia ya penalti na Aaron Cresswell.
Ndani ya dakika za majeruhi (Dakika ya 95) Leonardo Ulloa akaisawazishia Leicester City kwa penalti.
Leicester City imecheza michezo 34 na kujikusanyia pointi 73 na sasa inahitaji kushinda mechi mbili na sare moja ili isifikiwe na Tottenham yenye pointi 65 na michezo 33.
Leicester City pia inahitaji kushinda mchezo mmoja tu ili isifikiwe na Manchester City na Arsenal zenye pointi 6o na michezo 33. Manchester United yenye pointi 56 haina tena uwezo wa kuikamata Leicester.
Leonardo Ulloa wa Leicester akishangilia bao lake la kusawazisha dakika ya 95
Jamie Vardy akipiga bao la kwanza dakika ya 18
Jamie Vardy baada ya kufanya vitu vyake
Vardy anaenda chini baada ya kufanyiwa rafu na Angelo Ogbonna, lakini mwamuzi Jon Moss akamwadhibu kwa madai ya kujirusha
Vardy baada ya kulishwa kadi ya pili ya njano
Vardy akionyesha hasira
Comments
Post a Comment