LAURENT BLANC ameingizwa ghafla kwenye mbio za kuikochi Manchester United msimu ujao, nafasi ambayo kimahesabu ni kama tayari iko mikononi mwa Jose Mourinho.
Inasemekana kuna dalili kubwa ya bodi ya Manchester United kusapoti kuchukuliwa kwa Blanc anayeifundisha Paris Saint-Germain.
Blanc, sentahafu wa zamani wa Ufaransa, aliimalizia soka lake Manchester United kati ya mwaka 2001 na 2003.
The Sun la Uingereza linaandika kuwa sababu kubwa ya kutajwa kwa Blanc ni kumlinda Ryan Giggs.
Inaaminika kuwa Mourinho atatua United benchi lake lote la ufundi na kumpiga chini Giggs mwenye historia ya kipekee Old Trafford.
Hata hivyo kwa upande wa Blanc haitakuwa tatizo kwake kufanya kazi na Giggs aliyecheza naye pamoja kwa misimu miwili Manchester United.
Bado hakuna habari rasmi kuwa dili la Mourinho kwenda United limeyeyuka ambapo inaaminika kuwa makubaliano ya awali ya mkataba wa pauni milioni 6o yameshafanyika kwa Mreno huyo kumrithi Louis van Gaal.
Paul Scholes, Laurent Blanc na Ryan Giggs walipokuwa wakiitumikia Manchester United mwanzoni mwa miaka ya 2000
Comments
Post a Comment