Kocha wa kikosi cha Chelsea Guus Hiddink amesema kiungo wa timu hiyo Eden Hazard yuko kizani msimu huu.
"Msimu uliopita ulikua mzuri sana kwake, na kila kitu kilienda sawa lakini msimu huu kila kitu kwake kimekua kiza," alisema kocha huyo wa muda wa timu.
Katika msimu huu kiungo huyu amefunga mabao mawili tu katika michuano ya kombe la Fa huku akiwa hajazifumania nyavu katika michezo ya ligi kuu.
Hazard,mwenye umri wa miaka 25, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa (PFA) Mwaka 2015.
Kiungo huyu amebakiza miaka minne katika mkataba wake na miamba hao wa Stamford Bridge ila amekua akihusishwa na kuhama mwishoni mwa msimu huu.
Comments
Post a Comment