KIPA WA REAL BETIS AAHIDI KUISAIDIA REAL MADRID KUTWAA UBINGWA WA LA LIGA, ASEMA ATAIBANIA BARCELONA



KIPA WA REAL BETIS AAHIDI KUISAIDIA REAL MADRID KUTWAA UBINGWA WA LA LIGA, ASEMA ATAIBANIA BARCELONA

REAL BETIS itaifuata Sevilla Jumapili hii nyumbani kwao Ramón Sánchez Pizjuán katika mechi ya wapinzani wa mji mmoja - Seville derby au El derbi Sevillano, lakini kipaumbele cha kipa Antonio Adan ni mechi ijayo dhidi ya Barcelona.

Adan amesema anatumaini kuwasaidia waajiri wake wa zamani – Real Madrid katika mbio za ubingwa wa La Liga kwa kuwabania Barcelona watakapokutana nao nyumbani Benito Villamarín mwisho wa mwezi huu.

"Leo tunaifikiria Sevilla tu," alisema. "Baada ya hapo, mimi kama Madridista, niwe mkweli, natumaini tunaweza kuvuruga harakati za ubingwa za Barcelona."

Adan ameonyesha kuwa bendera yake ipo imara katika mlingoti wa Los Blancos, katika suala la nani atashinda taji la La Liga msimu huu. "Kama Real Madrid inaweza kushinda ligi, ityakuwa bora zaidi," alisema.


Comments