Barcelona walionekana wanaelekea kutwaa ubingwa wa pili mfululizo wa La Liga siku kadhaa tu nyuma, lakini kuanguka kwa kiwango chao kumewafanya sasa wawe sawa kwa pointi na Atletico Madrid kwenye kiti cha uongozi wa ligi, pointi moja nyuma ya Real Madrid.
Mnamo March 20, kikosi cha Luis Enrique kikiwa kinaongoza 2-0 vs Villareal, kikaruhusu wapinzani wao warudi mchezoni na kusawazisha magoli yote katika mchezo uliopigwa katika dimba la Estadio El Madrigal.
Wakati huo ilionekana ni kosa dogo Barca wamefanya na halitokuwa na athari kubwa katika mbio zao za ubingwa.
Hakuna ambaye aliyapa umuhimu mkubwa matokeo ya mechi ile.
Mechi zilizofuatia mbili za Wakatalunya hazikuwa nyepesi, walikuwa wanakutana na Real Madrid CampNou, kisha kufunga safari kwenda Estadio de Anoeta kucheza vs Real Sociedad.
Hata hivyo, kila mtu alitabiri Barca wangewaadhibu vijana wa Zinedine Zidane, na ilikuwa muda wa muafaka kwa Luis Enrique kulipa kisasi dhidi ya Real Sociedad baada ya kufungwa msimu na kidogo aikose kazi yake.
Haikuwa rahisi kama ilivyoadhaniwa, Barca wakapoteza mechi zote mbili na tangu hapo mambo yakazidi kuharibika.
Wakati Valencia walipoenda Camp Nou miezi miwili iliyopita, Barcelona waliwafunga magoli 7 katika nusu fainali ya Copa del Rey na kuelekea mchezo wa jana jumapili Barca walipewa nafasi ya kuweza kurejea katika kiwango chao.
Barca walionekana kuimarika katika mchezo wa jana, lakini walikuwa ni Valencia waliorudi kwenye ubora wao ambao walihakikishia Barcelona anaangukia pua kwene mchezo wa 3 mfululizo wa ligi, mara ya kwanza tangu mwaka 2003.
Kinachoikuta Barcelona msimu huu, kinaelekea kufanana na kilichoikuta Real Mallorca msiku wa 1998/99, Real Mallorca walipoteza uongozi wa pointi 9 na kuiacha Barcelona ya Louis Van Gaal kwenda kushinda ubingwa wa ligi msimu huo.
Huku kukiwa kumebakiwa mechi 5 kabla ya msimu kumalizika – kwa hakika Barcelona hawatotaka kupata matokeo mabaya tena, wanaweza kujikuta wamegeuka Real Mallorca ya msimu wa 1998/99 na Atletico au Real Madrid wakawa Barca ya msimu huo, kwa kutwaa La Liga baada ya kuachwa nyuma kwa pointi nyingi na viongozi wa ligi kabla ya kuwafikia na kuwazidi
Comments
Post a Comment