KANE HAKAMATIKI KWA KUTUPIA NYAVUNI EPL


KANE HAKAMATIKI KWA KUTUPIA NYAVUNI EPL

Harry Kane 4

Harry Kane alikuwa miongoni mwa nyota wakati Spurs ikipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke jana usiku kwenye dimba la Britania baada ya kuifungia timu yake magoli mawili na kuendeleza ubora wake kwenye ligi msimu huu.

Inafurahisha kuona jamaa alianza ligi kwa ukame wa magoli katika mechi kadhaa na baadhi ya watu kuanza kumsema yeye ni mchezaji wa ku-shine kwa msimu mmoja. Mshambulizi huyo wa England ameendelea kujitengenezea soko na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakao gombewa kwa mkwanja mrefu wakati wa usajili wa dirisha la majira ya joto.

Bayern Munich na Real Madrid inasemekana kuwa ni klabu mbili kubwa zinazofukuzana kumsaini lakini pia inasemekana Aston Villa wanataka kuuza washambuliaji wao wote na kuvunja benki kwa ajili ya kuinasa saini ya mpachika mabao huyo.

Magoli yake mawili ya jana dhidi ya Stoke yamemfanya afikishe jumla ya mabao 24 na kuongoza orodha ya wapachika mabao akifatimwa na Jamie Vardy wa Leicester mwenye magoli 22.



Comments