JOSE MOURINHO bado ana matumaini kwamba atakuwa kocha wa Manchester United mwisho wa msimu na ameripotiwa kupanga kufanya usajili wa mastaa watano kiangazi hiki.
Kocha huyo Mreno amekuwa na matumaini ya kutua Old Trafford baada ya msimu mbovu chini ya Louis van Gaal ambaye pia anaamini kuwa ataendelea kulinda kibarua chake.
Kwa mujibu wa mtandao wa ESPN, Mourinho anaamini mipango yote ya yeye kutua Old Trafford ipo kwenye mstari na kilichobakia ni suala la muda tu.
Majuzi akiongea na Sky Sports, Mourinho alisema msimu ujao atakuwa na timu mpya na kwamba matarajio yake kuendelea kufundisha Premier League.
Comments
Post a Comment