Skip to main content

JOSE MOURINHO ATAKA KUMSAJILI LEWANDOWSKI, NI MANCHESTER UNITED?



JOSE MOURINHO ATAKA KUMSAJILI LEWANDOWSKI, NI MANCHESTER UNITED? JOSE MOURINHO anataka kumsajili Robert Lewandowski.

Kocha huyo wa Kireno anapewa nafasi kubwa ya kumrithi Louis van Gaal ndani ya Manchester United msimu ujao iwapo Ed Woodward ataamua kusitisha kibarua cha Van Gaal.
Na sasa utashi wa Mourinho  katika usajili wake wa kwanza unaweza kuwa ni wa Lewandowski - hiyo ni kwa mujibu wa ujumbe wa simu ya mkononi aliomtumia mchezaji huyo miaka mitatu iliyopita.
Manchester Evening News inadai Mourinho alimtumia ujumbe huo mshambuliaji huyo wa Bayer Munich (enzi hizo akiichezea Borussia Dortmund) baada ya kufunga mara nne dhidi ya Real Madrid kwenye Champions League mwaka 2013. Mourinho ndiye aliyekuwa kocha wa Real Madrid kipindi hicho.
"Nataka ujiunge nami katika klabu yoyote nitakayokwenda"
"Nataka ujiunge nami katika klabu yoyote nitakayokwenda," ulisomeka ujumbe huo wa Mourinho.
Lewandowski  mwenyewe alikiri kuwa hilo lilikuwa ni jambo la kusisimua sana kwa kocha mkubwa kama Mourinho kumtumia ujumbe ule.
Inaeleweka kuwa Lewandowski yupo kwenye rada za Manchester United na Real Madrid.


Comments