Joe Hart ameendelea kuipa matumaini Manchester City ya kufika hatua ya fainali ya Champions League kwa mara ya kwanza baada ya kuokoa michomo miwili ya hatari wakati wa mchezo wa kwanza wa nusu fainali dhidi ya Real Madrid uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.
Ikicheza bila striker wake nyota Cristiano Ronaldo ambaye yuko nje kwasababu ya majeruhi, Real Madrid walifanya mashabulizi machache yenye uhai langoni mwa City hadi dakika za mchezo huo zinamalizika.
Dakika ya 20, Jese alipiga mpira kichwa ambao uligonga 'mtambaa panya' wa goli ya City kabla ya Hart kuokoa michomo ya Pepe na Casemiro iliyotokana na mipira kona.
Hart alionesha uwezo wa hali ya juu kuokoa kwa mguu mpira wa kichwa uliopigwa na Casemiro lakini baadaye alimnyima Pepe goli akiwa umbali wa mita tano kutoka lilipo goli, Hart amekuwa sababu ya City kusafiri kwenda Hispania wiki ijayo huku ikiwa na clean sheet.
Nafasi ya City kupata bao ilikuwa ni pale ambapo dakika za lala salama ambapo Kelvin de Bruyne alipiga mpira wa adhabu ndogo lakini uliokolewa kwa ustadi na golikipa wa Real Madrid Keylor Navas.
Hiyo ndiyo ilikuwa save pekee ya maana iliyofanywa na Navas kutokana na timu zote kutofanya mashambulizi makali kila mara golini kutokana na mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa kuwa ni ya kawaida.
City watakuwa na faida ya kuizuia Real kupata goli la ugenini lakini wawakilishi hao pekee wa England kwenye michuano ya Champions League bado wanakazi kubwa ya kufanya ili kufika hatua ya fainali itakayopigwa Milan May 28 mwaka huu.
Man City kushindwa kufunga goli kwenye uwanja wa nyumbani kutakifanya kikosi cha boss wa zamani wa Real Manuel Pellegrini kuhakikisha kinapambana kupata ushindi kwenye uwanja wa Bernabeu mahali ambapo kikosi cha Zinedine Zidane hakijaruhusu goli kwenye michuano ya Champions League msimu huu.
Real Madrid bila Cristiano Ronaldo
Taarifa za kwamba Ronaldo hatocheza mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na nyamana za paja zilikuwa njema kwa City kabla ya mchezo wao wa kwanza wa nusu fainali ya Champions League.
Wakicheza bila ya mfungaji wao mwenye magoli 47, kikosi cha Real ambacho kimefunga magoli 133 kwenye mechi 46 zilizopita msimu huu kilionekana kupambana kutengeneza nafasi za kufunga.
Gareth Bale akicheza kwa mara ya kwanza kwenye ardhi ya England tangu aliponunuliwa na Real Madrid kutoka Spurs kwa kitita cha £85m mwaka 2013, hakuweza kutema cheche bila ya uwepo wa Ronaldo.
Mara kadhaa Bale alimtoka Gael Clichy kutoka winger ya kulia lakini alishindwa kupiga pasin za mwisho kuwatafuta wachezaji wenzake hata alipoamua kumalizia mwenyewe bado umaliziaji wake haukuwa wa ubora uliozoeleka.
Nafasi nzuri za Real zilikuwa ni za mipira iliyokufa kutokana na kupata wakati mgumu kuwafungua City katika open play.
Safu ya ushambuliaji ya City inakazi ya ziada kwenye mchezo wa marudiano
City walikosa msaada kutoka kwa David Silva baada ya kulazimika kutoka uwanjani kabla ya half-time ambaye alikuwa akisaidia kupeleka mipira mingi kwa Aguero.
Sergio Aguero alikuwa chini ya ulinzi mkali hali iliyopelekea kufanikiwa kupiga shuti moja tu golini ambalo alilipiga akiwa nje kidogo ya box muda mchache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid sasa amefikisha mechi 13 alizocheza dhidi ya Real Madrid kwenye maisha yake ya soka huku akiwa hajawahi kufunga goli hata moja dhidi yao, lakini anaweza akapata nafasi nyingine Jumanne ya May 4.
Safu ya ushambuliaji ya City ianatakiwa kufanya kazi ya ziada kwenye mchezo huo wa marudiano.
De Bruyne ambaye alianza kucheza katika nafsi kama namba 10 alilazimika kwenda kucheza upande wa kushoto baada ya Silva kuumia, alikuwa na uhai mkubwa kwenye kikosi cha City pamoja na Jesus Navas ambaye mara kadhaa alikuwa akiingia ndani kutokea upande wa kulia
Man Of the Match
Alifanya kazi ya ziada mapema kipindi cha pili alipodaka mpira wa kichwa uliopigwa na Sergio Ramos lakini mlinda mlango huyo wa kimataifa wa England kwa mara nyingine aliisaidia timu yake kwa kucheza mara mbili mipira ya adhabu ndogo dakika za mwishoni.
Comments
Post a Comment