Na David Wambura
Ma-football legends wengi wamewahi kupita kwenye mchezo huu pendwa na kuacha alama zao, Pele na tik-taka, Diego Maradona na goli la 'mkono wa Mungu', Zidane na 'zizou', Johan Cruyff na mafanikio yake Barca kama kocha na total football yake ambayo imekuja kuzaa tik-taka tunayoiona kwa Pep Gurdiola na baadaye kama mchezaji na style yake maarufu 'Cruyff turn', Frans Beckbaur Kaizer aliye define style ya beki wa kisasa wakati ule maarufu 'sweaper' na mataji yake kama mchezaji na baadaye kocha kwa Bayern na Ujerumani hadi mafanikio ya miaka 26 ya Sir Alex Ferguson ndani ya United na style yake maarufu ya Fergie time, hao ni watu wazito kwenye soka ambao kwa nyakati tofauti wamewahi acha arama (legacy) itakayoishi daima miongoni mwa wapenda soka duniani kwa miaka mingi ijayo.
Ila 'arguably' hakuna aliyewahi fanya mapinduzi ya kweli ya kimfumo na kiutawala ndani ya vyombo vikubwa vya kuongoza mpira kama mtu aliyezaliwa Dec 1 miaka 52 iliyopita nchini Ubelgiji bwana Jean marc Bosman, japo mapinduzi tajwa hayakuja kirahisi kwani yalimghalimu pakubwa kama tutakavyoona mbele.
Kwa wale ambao hawajapata picha bado ya kile nachojaribu kukieleza huyu ndiyo mchezaji ambaye kwa ujasili wake alifanikiwa kuleta mapinduzi kwenye mikataba ya wachezaji wanaokua wamemaliza mikataba yao kua huru (free agent) kusaini klabu yeyote wanayoitaka na badala ya klabu kupewa pesa ya usajili kama ilivyokua awali sasa pesa hiyo wanapewa wachezaji maarufu kama Bosman ruling.
Kabla ya hapo klabu zilikuwa bado zina nguvu hata kwa wachezaji waliokua wamekwisha maliza mikataba yao na kila walipohama bado klabu zilikua zinadai na kulipwa fedha za usajili kutoka kwa klabu mpya anayohamia mchezaji husika, tofauti na ilivyo sasa ambapo pesa hizo sasa anapata mchezaji kama inavyoitwa sasa signing fees, kabla ya ushindi wake mwaka 1995 sheria na kanuni za UEFA zilikua hazimpi mchezaji uhuru huo.
Story ilianza hivi, Bosnan hakuwa mchezaji mwenye kipaji cha kutisha kama kina Pele na Cruyff ila ni mchezji unayeweza sema angeweza timiza ndoto ya kuwa mchezji wa kulipwa daraja la kati kwa dalili alizoonesha kabla ya mambo kumwendea kombo, kwani katika umri wa miaka 18 alikuwa ameweza kutoboa timu ya kikosi cha kwanza ya RFC Liege akitokea timu ya Standard liege na katika umri wa miaka 20 alikua amefanikiwa kucheza mechi ishirini za timu ya taifa za makundi tofauti ya umri wake, sio mbaya kabisa kwa mchezaji wa umri wake mambo yalionekana kwenda kwenye mstari
Shida ilikuja pale timu aliyokua akiichezea wakati huo ya RFC Liege kupata matatizo ya kiuchumi huku akiwa amemaliza mkataba wake, klabu ikiwa haina uwezo tena wa kumlipa mshahara wake wa awali walitaka muongezea mkataba ambao wangeweza kumlipa robo tu ya kile alichokua analipwa awali, Bosman akawaambia msinitanie, wakati wakiwa bado kwenye mgogoro ikatokea klabu nchi jirani ya Ufaransa inaitwa Dunkerque iliyokua tayari kumlipa mshahara aliokua anautaka Bosman.
RFC liege kuona hivyo na njaa zao wakati huo wakaleta nongwa huendi mpaka tulipwe chetu, tena madai yao walipwe na Dunkerque mara nne ya kile walikua wanamlipa Bosman, kumbuka tu Bosman mkataba wake ulishaisha na RFC Liege lakini kama nilivyosema awali sheria za UEFA zilikua zinaruhusu RFC Liege kufanya unyama huo na kwa wakati ule kwenye dunia ya mpira hilo lilikua jambo la kawaida kasoro kwa mmoja tu Bosman.
Ikiwa ni mwaka 1990 kupitia kwa mwanasheria wake aliamua kuwashitaki klabu ya RFC Liege, Belgium FA na UEFA kwenye mahakama ya ECJ (European Court of Justice) kwa kosa la kuzuia kwa hila biashara halali kufanyika kitaalam wanaita "prejudice entrainment of legitimate trade", ulikuwa uamuzi wa kishujaa kukishitaki chama cha soka cha nchi yake na UEFA na kama nilivyosema uamuzi huo uliambatatana na gharama kubwa, mwanasheria wake akitegemea ingeichukua ECJ wiki mbili pekee kufikia maamuzi lakini iliwachukua miaka mitano kufikia verdict toka mwaka 1990-1995 kipindi ambacho Bosman kama mchezaji alipaswa kupiga hatua kufikia malengo yake kisoka, haikuwa hivyo kilikua kipindi cha majanga makubwa kwake.
Akiwa kafungiwa kucheza nchini Ubelgiji na nchi wanachama waliochini ya UEFA, njia pekee aliyokua nayo ilikua kucheza ligi za madaraja ya chini yasiyochini ya UEFA ambako hata huko anadai hakua kivutio sana kwa wenyeviti wa vilabu hivyo vidgo alivyojaribu kuvichezea kutokana na songombingo lake na UEFA licha ya kufanikiwa kucheza hapa na pale madaraja ya chini Ufaransa hilo halikumridhisha Bosman mchezaji aliyekuwa anamatarajio makubwa kisoka, Bosman aliandamwa na msongo wa mawazo hali iliyopelekea kuwa na matatizo ya kiakili, kunywa kuliko pitiliza kuliko pelekea kuachwa na mpenzi wake na baade kufungwa jela.
Mpaka verdict (maamuzi) ya kesi yake yanatoka mwaka 1995 alikua kachoka mbaya, akiwa katoka kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, amekimbiwa na mpenzi wake, msongo wa mawazo huku akiwa na majukumu ya kutunza watoto wake watatu alilazimika kurudi kijijini kuanza maisha mapya na hivyo ECJ walivyomtaka akubali faini ndogo kwa ajili ya usumbufu wake alioupata kwa miaka mitano kwa umaskini wake hakuwa na jeuri ya kuzikataa Swiss franc 350,000 alizolipwa kama fidia.
Huku akiwa hana mawazo ya nini cha kufanya, kipindi ambacho alikuwa akishuhudia rundo la wachezaji waliowahi faidika na maamuzi ya kesi yake kama kina Sol Campbel, Beckham, Mc Manaman list ni kubwa mno wakiendelea kuneemeka aliamua kuanzisha mradi wa kuuza T-shirt, akiamini wachezaji matajiri waliofaidiaka na maamuzi yale yaliyomuumiza yeye wangemuunga mkono kwa kuzinunua mwisho wa siku ziliishia kununuliwa na mtoto wa mwanasheria wake pekee huku mzigo mzima ukimdodea baada ya wachezaji kumfungia vioo.
Lakini hapa ndipo walau FifPro chama kinachojihusisha na maslahi ya wachezaji wa kulipwa duniani walipoguswa na kuamua walau kumpa mkono asiendelee kuanguka walimtafuta wakampa ubalozi wa kutetea haki za wachezaji na sasa Bosman anadai anajipanga kwenda kumalizia kudai sehemu ya pili ya madai yake, akisema hata Bosman ruling ya sasa haikua exactly ya kile alichokua anakimaanisha.
Bosman huku akiwa hana hata uwezo wa kulipia king'amuzi (subscribtion) cha kuangalia mpira wa wachezaji wa sasa wanaovuna pesa nyingi kutokana na mabomu aliyoamua kujifunga mwaka 1990, anadai maamuzi ya mwaka 1995 al-maalufu kama Bosman ruling yamemfaidisha kila mchezaji isipokua yeye pekee na anaedhani anatania aende akamuonyeshe Bank statements.
Tupige story na David Wambura
Comments
Post a Comment