JAVIER HERNANDEZ 'Chicharito' ameionya Manchester United kwamba haitopata mbadala wa Sir Alex Ferguson katika kipindi cha miaka 100 ijayo, wakati mustakabali wa kocha wa sasa, Louis van Gaal ukiendelea kuwa majadala.
Kibarua cha Van Gaal Old Trafford kinaripotiwa kuwa hatarini, wakati kikosi chake kikiwa nafasi ya tano katika Premier League – pointi tano nyuma ya mstari wa timu nne za juu kwenda Champions League.
Jose Mourinho na Ryan Giggs wanatajwa kuwa warithi wa Mholanzi huyo, lakini Chicharito – ambaye aliuzwa Bayer Leverkusen na United mwanzo wa msimu – anahisi klabu hiyo daima itahangaika kurejea mafanikio yaliyofikiwa chini ya Ferguson.
"Van Gaal ni kocha mzuri kwa ukweli," Chicharito aliiambia Sky Sports. "Ana njia zake kama ilivyo kwa makocha wote duniani.
"Huwezi kupata Sir Alex Ferguson mpya katika miaka 50 ijayo au 100 kwa sababu alikuwa wa kipekee. Alikuwa maalum.
"Van Gaal anaweza kufanya hivyo, lakini katika soka muda na matokeo vinazungumza kama yeye ni mtu muhimu au la."
Comments
Post a Comment