HUYU NDIYE BEKI WA KUSHOTO WA JUVENTUS ANAYEWANIWA NA MACHESTER UNITED … ni Alex Sandro mwenye thamani ya pauni mil 40
MANCHESTER UNITED imeripotiwa kuangalia uwezekano wa kumsajili beki wa kushoto wa Juventus, Alex Sandro, ambaye alijiunga na miamba hiyo ya Italia msimu uliopita.
Kwa mujibu wa tovuti ya Tuttomercatoweb.com ya Italia, Juventus haiko tayari kupokea ofa ya chini ya pauni milioni 36.6 kwa ajili ya Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 25.
Sandro ana kipengele kinachomruhusu kuondoka kwa pauni milioni 40 na Juventus imeweka wazi kuwa iwapo United inataka saini ya nyota huyo ni lazima iweke mezani pauni milioni 40.

Comments
Post a Comment