HIKI NDIYO KIKOSI CHA 11 BORA YA PREMIER LEAGUE 2016 ...Arsenal na Man United zambulia moja moja, Man City, Liverpool patupu
CHAMA cha Wachezaji wa Kulipwa England (PFA) kimetangaza kikosi chake cha mwaka 2016 ambapo mastaa kutoka Manchester United, Arsenal, Tottenham, Leicester na West Ham wametajwa kuunda kikosi cha kwanza cha wachezaji 11.
Toby Alderweireld, Danny Rose, Dele Alli na Harry Kane wote wanaiwakilisha Spurs katika kikosi hicho, wakati Foxes ikitoa mashujaa wake, Wes Morgan, N'Golo Kante, Riyad Mahrez na Jamie Vardy.
Licha ya Arsenal kupotea katika mbio za ubingwa wa Premier League, Hector Bellerin amechaguliwa katika beki ya kulia na Dimitri Payet naye amejumuishwa ingawa amekosa kuisaidia West Ham sehemu kubwa ya msimu kutokana na kuwa majeruhi.
Kwa mshangao, kipa wa Manchester United, David De Gea ni chaguo katikati ya milingoti miwili baada ya kipindi kigumu katika ushiriki wa timu yake chini ya Louis van Gaal.
Comments
Post a Comment