Bosi wa Southampton Ronald Koeman yuko              miongoni mwa majina ya makocha wanaotajwa kumrithi  Arsene              Wenger ndani ya Emirates Stadium.
        Wenger amebakiza mwaka mmoja kwenye              mkataba wake Arsenal lakini sasa kumeibuka shinikizo kubwa              linalotishia kung'oka kwa kocha huyo mwishoni mwa msimu huu.
        Kwa mujibu wa The Sun la Uingereza,            Arsenal imeanza kumulika watu wanaofaa kumrithi Wenger ambapo            Koeman anaongoza orodha hiyo.
        Koeman amefanya kazi nzuri Southampton            tangu alipomrithi Mauricio            Pochettino mwaka 2014.
        Mdachi huyo naye anaingia mwaka wa mwisho            katika mkataba wake Southampton lakini klabu hiyo inataka            kumpa mkataba mpya wa muda mrefu.
        Kocha wa Atletico Madrid - Diego Simeone na            Laurent Blanc wa PSG nao ni miongoni wa mabosi wanaotajwa            kutua Emirates Stadium.
        
Comments
Post a Comment