HATIMAYE FAMILIA YARIDHIA NDANDA KUZIKWA DAR ES SALAAM JUMATANO ...safari ya Congo yafutwa



HATIMAYE FAMILIA YARIDHIA NDANDA KUZIKWA DAR ES SALAAM JUMATANO ...safari ya Congo yafutwa

Kikao cha familia ya Ndanda na ubalozi wa Congo (DRC) hapa Tanzania, kwa pamoja wamekubaliana kubadili wazo la kwenda kumzika Ndanda huko Congo na sasa atazikwa Dar es Salaam siku ya Jumatano (tarehe 13 mwezi huu).

Msiba uko pale pale Kinondoni Hananasif katika nyumba inayomilikiwa na ubalozi wa Congo (DRC).


Kardinal Gento ameiambia Saluti5 kuwa hii sasa ni taarifa ya mwisho kuhusu wapi atakapozikwa Ndanda na hakutakuwa na badiliko lingine na kwamba ndugu wa marehemu walioko Congo wanajiandaa na safari ya kuja Tanzania kuzika.

"Tumeamua hivyo baada ya kujiridhisha kuwa Ndanda ana marafiki wengi zaidi hapa Tanzania ambao amekuwa akiishi nao kama ndugu," alisema Kardinal.


Comments