THEO WALCOTT yu tayari kuondoka Arsenal kiangazi hiki kama hatapata nafasi ya kucheza katika fainali za michuano ya mataifa ya Ulaya - Euro 2016.
Staa huyo amezidi kupata hofu juu ya hatima yake kutokana na kukosa muda zaidi wa kucheza katika kikosi cha Arsenal, na akasema kama hatakuwamo katika kikosi cha Roy Hodgson kitakachobeba bendera ya England katika Euro 2016, atafikiria kuondoka Emirates.
Kwa mujibu wa mtandao wa Bleacher Report, hakuonekani kuwapo uwezekano kwa Hodgson kumchagua staa huyo mwenye umri wa miaka 27 katika kikosi cha England.
Walcott amejikuta akipoteza nafasi yake mbele ya kinda wa miaka 19, Alex Iwobi katika wiki za karibuni na sasa ana wasiwasi juu ya mustakabali wake.
Arsenal inaaminika kuwa tayari kupokea ofa kwa ajili ya Walcott ambaye kwa sasa anavuta mshahara wa pauni 140,000 kwa wiki.

Comments
Post a Comment