Hat trick ya Ronaldo Yaingizia Madrid bilioni 20, na hizi hapa ndio rekodi alizoweka jana – bado goli 4 amfikie Pele
Usiku wa jana ulikuwa wa Cristiano Ronaldo – magoli yake matatu yakaiwezesha Real Madrid kusonga hatua ya nusu fainali kwa mara 6 mfululizo.
Kingine kikubwa pamoja na kuivusha timu yake – magoli hayo matatu ya Cristiano Ronaldo yameingiza bank kiasi cha £6.8MILLION zaidi ya billioni 20 za kitanzania.
Hii ni fedha ambayo Real Madrid wanapata kwa kufanikiwa tu kuingia kwenye hatua ya nusu fainali ya UEFA Champions League.
Ripoti zinaeleza mchanganuo wa fedha hizo ni 5.6m kwa kuingia nusu fainali — na £1.2m kwa kushinda mechi ya jana usiku.
Mabingwa wa mara 10 wa Champions League walifungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza huko Ujerumani, kabla ya hat trick ya Ronaldo jana kuwaingiza katika listi ya vilabu 9 tu vilivyowahi kufanikiwa kufuzu hatua inayofuata baada ya kukubali kipigo cha 2-0 au zaidi katika mchezo wa kwanza wa Champions League.
Magoli yake ya jana yamemfanya atimize magoli 16 msimu huu – hii ni mara ya pili kwake kufanikiwa kuvuka magoli 15 kwa msimu mmoja wa Champions League – hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kufanya hivi.
Pia hat trick ya jana usiku imemfanya atimize hat trick yake ya 41 katika maisha yake ya ushindani wa soka – pia amefanikiwa kumfikia Lionel Messi ambaye mpaka jana ndio alikuwa anaongoza kaa kufunga hat trick nyingi kwenye Champions League – hat trick 5.
Ronaldo sasa anakuwa mchezaji pekee kufanikiwa kufunga hat tricks 3 katika msimu mmoja.
Kingine kikubwa – Ronaldo mpaka sasa ana magoli 46 msimu huu katika mashindano yote – amebakisha magoli 4 tu afikie rekodi ya Pele ya kufunga magoli 50 au zaidi kwa misimu 6 mfululizo.
Comments
Post a Comment