Nyota wa Real Madrid Gareth Bale amezima hisia kuwa amewahi kukwaruzana na Cristiano Ronaldo kwa kusisitiza kuwa mchezaji mwenzake huyo amemsaidia sana katika kuzoea maisha ya Hispania.
Baadhi ya vyombo vya habari mara kadhaa vimekuwa vikimhoji Bale juu ya uhusiano wake na Ronaldo uwanjani na nje ya uwanja, lakini raia huyo wa Wales hakuwa lolote zaidi ya kusema kamwe hawakuwahi kuwa na mzozo.
Bale alitua Real Madrid mwaka 2013 akitokea Tottenham kwa ada ya rekodi ya dunia ya pauni milioni 86, lakini mara kadhaa ilidaiwa kuwa aliwahi kushutumiwa na Ronaldo kwa uchoyo wa pasi.
Katika mahojiano yake na The Times, Bale alisema: "Ronaldo anazungumza Kiingereza na alinisaidia sana nilipofika hapa. Tulikuwa pamoja kwenye Premier League na hivyo ilikuwa rahisi kwetu kuwa na mawasiliano mazuri.
"Vyombo vya habari vimekuwa vikisema vitu vingi ambayo wakati mwingine havikuwahi kutokea. Sikuwahi kulumbana nae. Ni mtu mwema uwanjani - kila mtu anajua hilo, wakati mwingine watu wanamtafsiri ndivyo sivyo. Hatuna tatizo hata kidogo."
Gareth Bale (katikati) akishangilia na Cristiano Ronaldo (kulia)
Bale na Ronaldo
Bale (kulia) anasema hana bifu na Ronaldo (kulia)
Comments
Post a Comment