Umewahi tilia mashaka Uhalali wa Fergie kupata cheo cha 'U-sir'? japo ukweli unabaki alistahili kupata hicho cheo kwa mafanikio ya kipekee aliyoyapata mwaka 1999 (dinstinctive achievements) moja ya kigezo kinachotumika kumtunuku mtu U-sir kwenye visiwa vya Uingereza ila amini nachokwambia wapo waliotilia mashaka kupewa heshima hiyo na wenye mashaka hayo wana hoja zenye mashiko
Moja ya hoja zao ni kwamba si kocha wa kwanza kwenye visiwa hivyo kupata mafanikio ya kipekee, unamkumbuka Brian Clough kocha aliyemuibua Roy Keane na aliyewahi chukua kombe la ligi Championship wakati huo baada tu ya kua amaeipandisha timu kutoka daraja la pili akiwapiku mabingwa watetezi Liverpool kwa pointi saba na akiwafunga mechi ya fainali Carling Cup mwaka 1978-79.
Alichukua UEFA Champions League mara 2 mfululizo akiwa na club ndogo ya Nottigham Forest msimu wa 1978-79 na 1979-80, huyu ni moja ya makocha ambao wamewahi cheza mechi zaidi ya 40 bila kufungwa, kocha aliyewahi chukua ubingwa wa ligi akiwa na vilabu viwili tofauti, mtu ambaye enzi za uchezaji wake alikua striker wa kutisha mwenye wastani wa magoli 204 kwenye mechi 222 kabla ya kustaafu mpira akiwa na umri mdogo baada ya kupat 'cruciate ligament injury'.
Vipi kuhusu Billy Shankly na makombe yake pale Liverpool? ambaye kutokana na nafasi ziwezi elezea CV yake, mbona hawa walirukwa U-sir?
Watia mashaka hao wanaendelea kuonesha mashaka yao wakihusisha cheo hicho na uhusiano wa karibu uliokuapo kati yake na Tony Blair kiongozi mkuu wa chama cha Labour wakati huo, mtu wa karibu kabisa wa Tonny Blair wakati huo bwana Alistair Campbell anasema Fergie aliharakishwa kua 'knighted' (kupewa U-sir) kutokana na urafiki uliojengeka kati yake na Tonny Blair wakati huo.
Urafiki ulioanza baada ya Fergie kuwa anatoa darasa kwa Tonny Blaiar juu ya namna ya kudhibiti watu wennye majina makubwa na wasioambilika kirahisi (watu wenye big egos) waliokua wanamsumbua Blair enzi hizo ndani ya chama, Fergie alifanya hivyo kwa kutumia uzoefu wake wa namna alivyoweza kuwadhibiti wachezaji wakorofi wenye majina makubwa na wasioambilika kirahisi kama Erick Cantona na Andy Cole.
Akitolea mfano wa Cantona na Andy Cole Fergie alisema, katika kuhakikisha wachezaji wa dizaini hiyo wanajua nani ni boss kati yake na wao wakati wa kuwasainisha mikataba alikua anawaita kwenye chumba kidogo cha hoteli kisicho na hadhi yao lengo likiwa kutaka kuwaonyesha yeye ndiyo boss wao na anaweza kuwaita popote na kuwaambia chochote wakafuata.
Kitu cha pili alichogusia ni kwamba, unapokuwa na watu wa dizaini hii njia nyingne rahisi ni kuhakikisha kila mtu anajua majukumu yake kwenye timu na anayatimiza. Wakati wote ajue timu inaanza halafu yeye anafuata, hakuna mchezaji mkubwa kuliko club na kwamba boss ni mmoja tu 'FERGIE' hivyo mnyetishaji huyo anadai kasi ya kuharakishwa kuwa knighted (kupewa u-sir) iliongezeka mara dufu baada ya mafabnikio ya Fergie mwaka 1999 na kwamba nyuma ya pazia urafiki huo ulicheza role kubwa.
Baada ya hayo sasa tujielekeze kwenye hoja nyingne ya msingi, kwamba marafiki hao kwa nyakati tofauti kuondoka kwao kumeacha madhara makubwa kwa taasisi walizokua wanaziongoza, Fergie kwa Man United na Blair kwa chama cha Labour.
Toka Fergie ameondoka Man United, wamepita warithi wawili lakini mambo hayajatengemaa, alianza Moyes msimu mzima akashika nafasi ya 7 bila hata kikombe cha chai, amekuja Van Gaal kocha mzoefu ambaye mabosi wake waliamini timu imetua mahala salama lakini ni msimu wa pili sasa hakuna kombe na bado kiwango cha timu ni kama homa ya vipindi, timu chini ya LVG imekua ikiwapa mashabiki wake 'emotional roller coaster' kama ambavyo wamekua wakisikika wakisema leo kule kesho huku.
Hali kama hiyo imekisibu chama cah Labour ambao toka ameng'oka Blair wamepita viongozi wawil Alan Kobyn na Gordon Brown lakini wamesha poteza chaguzi tatu tofauti.
Ukifikiria kwa makini unagundua tatizo ni moja tu lililopelekea matokeo husika, tatizo ambalo ni mara chache sana kulikuta linatokea nchi za wenzetu wa dunia ya kwanza, mara nyingi tatizo kama hilo tumelizoea nchi za Afrika na wenzetu wa dunia ya tatu. Tatizo la kujisahau na kujikuta mnajenga mtu na si taasisi, lakii hapa chama cha Labour na na Man United walijisahau na kujikuta wanafanya kile ambacho kilifanywa na FIFA enzi za Blatter.
Kwa muda mwingi Fergie na Tonny Blair walitumia udhaifu wa taasisi zao wa kuwaamini sana kujijenga wao zaidi ndani ya taasisi kuliko kuzijenga taaasisi zenyewe, Fergie alikuwa zaidi ndani ya Utd kuliko United ilivyokua ndani ya Fergie, kibabu Fergie aliijenga United kwenye taswira yake na klabu iliendeshwa kupitia mishipa ya damu yake.
Wachezaji aliokua akiwanunua ni wale waliokua wanaweza kumpa matokeo yeye kama yeye kwa kutumia mbinu anazozijua vema yeye mwenyewe ndiyo maana ni rahisi sana kocha mwingine akirithi wachezaji walewale haoni 'quality' ya kumpa ubingwa kwenye baadhi ya maeneo, tofauti na timu kama Real Madrid, Barca, Chelsea, PSG na nyingne zenye quality inayoweza mpa matokeo kocha yeyote bila ulazima wa kufanya mabadiliko makubwa kwa sababu quality tayari ipo.
Vivyo hivyo unaweza kusema juu ya Tonny Blair ndani ya Labour au FIFA chini ya Blatter. Hivyo binafsi nikiziangalia taasisi tajwa hapo juu zinavyoweweseka hua najua wale walioziacha wana lawama nyingi za kubeba juu ya mizimu yao inavyozitesa taasisi walizoziacha, japo mara kwa mara hilo huwa halisemwi ila naamini hata wao kimoyomoyo Fergie na Blair wanajua waliacha majumba bovu.
Karibu tuongee mbinu na David Wambura

Comments
Post a Comment